Snoop dogg athibitisha kuomba msamaha kwa mpwa wake Kendrick Lamar

Snoop dogg athibitisha kuomba msamaha kwa mpwa wake Kendrick Lamar

Snoop Dogg ameelezea kilichotokea hadi akashiriki wimbo wa Drake, “Taylor Made Freestyle,” uliotumia sauti za AI za msanii huyo wa West Coast pamoja na marehemu Tupac Shakur.

“Kilichotokea ni kwamba nilifanya post ya kolabo na mtu. Wakati nafanya hivyo, sihusikilizi muziki, naona tu ‘Gin & Juice’ kwa sababu ni biashara yangu,” alisema Snoop. “Nilivyopost, nilifikiri napost ‘Gin & Juice.’ Sikujua huu ni wimbo gani. Sijui muziki wa kila mtu.”

Baada ya muda, Snoop alipata ujumbe: “‘Mpwa hakupenda ulichochapisha.’ Nikasema, ‘Nimefanya nini?’ Wakanijibu, ‘Ulichapisha wimbo fulani.’ Nikajiuliza, ‘Wimbo gani?’ Nilipokwenda kuangalia ile post, nikaona ni Drake. Ndipo nikafuta, nikampigia Kendrick Lamar simu, nikamuachia ujumbe kwa sababu hakuweza kupokea. Alikuwa kazini akifanya mambo yake. ‘Mpwa, ni Uncle Snoop. Nimepata ujumbe. Naomba radhi. Nilikosea. Samahani.’”

Snoop pia alisisitiza kuwa hana mpango wa kujiingiza kwenye ugomvi wa mtu yeyote, isipokuwa ikiwa anasaidia kuumaliza.

Share: