
Kwa kuzingatia maelezo yaliyofichuliwa na vyombo vya habari na shirika la ujasusi wa kijeshi la Ukraine (SBU), operesheni ya hivi karibuni ndiyo yenye mafanikio zaidi kufikia sasa.
Bomu lenye uzito wa kilo 250 liliharibu jengo kuu la utawala la jiji hilo na kutandaza vyumba vitatu vya ghorofa. Waandishi wa habari kutoka chombo cha habari BBC Wamewasili eneo hilo siku moja baada ya bomu kupigwa, lakini moshi bado unaendelea kufuka. Kutoka nje kidogo ya mji, tunasikia sauti ya milio ya risasi : Wanajeshi wa Ukraine wakidungua ndege zisizo na rubani.
Rodynske iko karibu kilomita 15 kaskazini mwa mji uliozingirwa wa Pokrovsk. Urusi imekuwa ikijaribu kuliteka eneo hilo kutoka kusini , lakini vikosi vya Ukraine vimeweza kusitisha harakati za Urusi.
Kwa hivyo Urusi imebadilisha mbinu na kuchagua kuzunguka mji na kukata njia za usambazaji wa silaha na wanajeshi. Katika wiki mbili zilizopita, ikikabiliwa na kushindwa kwa juhudi za kidiplomasia za kufikia usitishaji mapigano nchini Ukraine, Urusi imezidisha mashambulizi yake, na kupiga hatua kubwa tangu mwezi Januari.