Siku ya pili ya kliniki ya rc makonda mkoani arusha inaendelea zaidi ya watu 950 walisikilizwa siku ya jana na kutatuliwa changamoto zao mbalimbali

Mkuu wa Mkoa anasisitiza kuwa kila Mwananchi anayefika hapo Ofisini kwake asikilizwe na wataalamu na watumishi

Leo ni siku ya pili ya Kliniki ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda, ikiwa na lengo mahususi la kusikiliza na kutatua kero na changamoto Mbalimbali za wananchi wa Mkoa wa Arusha pamoja na kupatiwa misaada mbalimbali ya kisheria kutoka kwa Mawakili wanaotoka Ofisi zaidi ya 75 zenye kutoa msaada wa kisheria mkoani Arusha wakiongozwa na Chama Cha wanasheria wa Tanganyika TLS.


Siku ya Jana zaidi ya watu 950 walifika, kusikilizwa na kutatuliwa changamoto zao mbalimbali na Mhe. Mkuu wa Mkoa anasisitiza kuwa kila Mwananchi anayefika hapo Ofisini kwake asikilizwe na wataalamu na watumishi wanaosikiliza wananchi wahakikishe wananchi wanaridhika na michakato ya kuwasikiliza na majibu wanayoyapata kutoka kwao.


Share: