Shirika linalosimamia usalama wa nyuklia (iaea) limeitaka iran kuacha kuwazuia baadhi ya wakaguzi wake

Shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia usalama wa nyuklia (IAEA) limepitisha azimio la kuitaka Iran kushirikiana kwa haraka na kutengua uamuzi wake wa kuwazuia baadhi ya wakaguzi wake.

Kuna wasiwasi kuwa Iran inajaribu kutengeneza silaha za nyuklia, tuhuma ambayo Tehran inakanusha.

Azimio hilo lililoandaliwa na Uingereza, Ufaransa na Ujerumani, lililopitishwa na baraza la mataifa 35 lilipigiwa kura na nchi 20, huku China na Urusi pekee zikipiga kura hiyo. Mataifa kumi na mawili yalijizuia na nchi moja haikushiriki kabisa kura hiyo.

Iran iliuita uamuzi huo "wa haraka na usio wa busara", Televisheni ya taifa ya Iran iliripoti.

Azimio hilo lililopitishwa katika mkutano wa robo mwaka mjini Vienna, lilisema Iran lazima itoe ushirikiano tena kwa haraka, kikamilifu na bila utata na IAEA.

Pia ilisema Tehran inapaswa kujibu maswali ya muda mrefu kuhusu athari za urani zilizopatikana katika maeneo mawili huko na kuruhusu baadhi ya wakaguzi wenye uzoefu mkubwa wa shirika hilo kurudi nchini humo.

Iran sasa inarutubisha uranium hadi 60% - karibu na 90% inayohitajika kwa daraja la silaha - wakati inaendelea kukusanya hifadhi kubwa ya uranium, kulingana na IAEA.

Hatua hiyo inalenga kuongeza shinikizo la kidiplomasia kwa Iran.

Share: