Sheikh wa mkoa wa arusha amuombea kheri rc makonda

Sheikh wa Mkoa wa Arusha Sheikh Shaaban Bin Juma Akiambatana na Viongozi wengine wa Baraza la Kiislamu Mkoa wa Arusha leo Mei 7, 2024 ameongoza sala Maalum ya kumuombea Kheri Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda ili aweze kufanikiwa kwenye Programu yake maalum inayoanza kesho Mei 08,2024.


Mkuu wa Mkoa Mhe. Paul Christian Makonda atakuwa na siku tatu Maalum za kusikiliza na kutatua Kero mbalimbali za Wananchi wa Arusha kuanzia Kesho Mei 8-10, Zoezi ambalo litafanyika kwenye Ofisi za Mkuu wa Mkoa Mjini Arusha.


Sheikh Shaaban Bin Juma amempongeza pia Mkuu wa Mkoa Mhe. Paul Christian Makonda kwa maono yake ya Kuja na Programu ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi, akisema programu hiyo ni sehemu ya kuhakikisha Arusha inakuwa na Amani, usalama na Matumaini ya kutosha kwa wananchi na wageni wanaofika Mkoani hapa.

Share: