Zaidi ya waandamanaji 300 waliuawa kufuatia maandamano ya kupinga upendeleo katika kutoa ajira
Waziri Mkuu nchini Bangladesh Sheikh Hasina ambaye amejiuzulu ameitoroka nchi hiyo kufuatia maandamano yanayoendelea nchini humo.
Hasina ambaye aliiongoza nchi hiyo tangu mwaka wa 2009 ametoroka kwa kutumia helikopita na kukimbilia katika mji wa Agartala nchini India.
Waandamanaji walivamia ofisi yake na na makazi yake katika mji Mkuu wa Dhaka huku ikisubiriwa hotuba kutoka kwa Mkuu wa Majeshi Jenerali Waker-Uz-Zaman.
Zaidi ya waandamanaji 300 waliuawa kufuatia maandamano ya kupinga upendeleo katika kutoa ajira.
Share: