Waisraeli wanaangalia ukweli kwamba Iran na Hezbollah hazijafanya bidii kama ambavyo wengine wanaweza kutarajia.
Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi nchini Iran IRGC kimesema maafisa saba wameuawa katika shambulizi la Israel dhidi ya jengo la ubalozi mdogo wa Iran katika mji mkuu wa Syria, Damascus.
Brig-Jenerali Mohammad Reza Zahedi, kamanda mkuu wa Kikosi cha wasomi cha Quds, na Brig-Jenerali Mohammad Hadi Haji-Rahimi, naibu wake, walitajwa miongoni mwa waliofariki, Serikali za Iran na Syria zililaani shambulizi hilo ambalo liliharibu jengo jirani na ubalozi wa Iran.
Jeshi la Israel lilisema halizungumzia taarifa za vyombo vya habari vya kigeni.Hata hivyo, limekiri kutekeleza mamia ya mashambulizi katika miaka ya hivi karibuni kwa kuyalenga makundi ambayo yana uhusiano na Iran nchini Syria na makundi washirika yenye silaha ambayo, yanayofadhiliwa na kupewa mafunzo na Walinzi wa Mapinduzi.
Mashambulizi ya Israel yameripotiwa kuongezeka tangu kuanza kwa vita huko Gaza mwezi Oktoba mwaka jana, kujibu mashambulizi ya kuvuka mpaka kaskazini mwa Israel yaliyofanywa na Hezbollah na makundi mengine yanayoungwa mkono na Iran huko Lebanon na Syria.
Lakini shambulio la Jumatatu litaonekana kama ongezeko kubwa la mashambulizi hayo.
Waisraeli wanaonekana kujaribu azma ya Wairani na washirika wao na kuashiria kwamba wana nia ya dhati ya kuongeza shinikizo kwa maadui zao.
Waisraeli wanaangalia ukweli kwamba Iran na Hezbollah hazijafanya bidii kama ambavyo wengine wanaweza kutarajia. Sasa wanataka kuona iwapo Iran na Hezbollah watachukua hatua yoyote dhidi ya Israel.