Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov amesema Urusi itafanya uchunguzi yenyewe kwakuwa wameshazoea
Serikali ya Urusi imekataa ofa ya Polisi wa kimataifa (Interpol) ya kuwasaidia kufanya uchunguzi kujua Wahusika Wakuu wa shambulizi lililoua Watu zaidi ya 130 Crocus City Hall Nchini humo.
Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov amesema Urusi itafanya uchunguzi yenyewe kwakuwa wameshazoea na wanazijua vizuri mbinu za Nchi za Magharibi na namna wanavyofanya upendeleo kwenye maswala ya uchunguzi.
“Sikumbuki kama Interpol walijitolea kutusaidia uchunguzi wa shambulizi la bomba la mafuta la Nord Stream (ambao ulikata njia kuu ya usafirishaji wa gesi kutoka Urusi hadi Ulaya ) ingawa tuliliomba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, kwahiyo hatutaki msaada wa uchunguzi wao kwenye shambulizi hili ili walete upendeleo wao