Serikali ya uingereza kupiga marufuku vapes ili kuzuiwa kutumiwa na watoto

Serikali ya Uingereza inatarajia kupiga marufuku matumizi ya Sigara za Kielektroniki ikiwa ni sehemu ya mipango ya kukabiliana na ongezeko la matumizi makubwa ya vijana katika uvutaji huo.

Takwimu za Shirika la kutoa Misaada la Action on Smoking and Health (Ash) limeema 7.6% ya Watoto wenye umri wa miaka 11 hadi 17 ni watumiaji wa mara kwa mara wa vifaa hivyo, takwimu ikiwa imepanda kutoka 4.1% ilivyokuwa Mwaka 2020.

Waziri Mkuu wa Uingereza, Rishi Sunak anatarajiwa kutoa tangazo hilo leo Januari 29, 2024.

Hatua hiyo inafuatia baada ya kutolewa kwa muongozo wa kutowauzia sigara wote ambao walizaliwa kuanzia Januari Mosi, 2009 ili kitengeneza kizazi kisichovuta sigara.

Mvuke wa Vapes hauna madhara makubwa kama ilivyo uvutaji wa sigara lakini inaelezwa unaweza kutoa kiasi kidogo cha kemikali zinazopatikana katika sigara.

Share: