Serikali ya uganda imesitisha zoezi la kutoa pasipoti mpya kutoka nje ya nchi

Chini ya miongozo mipya kutoka Ofisi ya Uhamiaji nchini Uganda, Waganda wanaoishi nje ya nchi watalazimika kuingia gharama za ziada kusafiri kurudi Uganda kwa ajili ya kubadilisha hati ya kusafiria.

Kulingana na Ofisi ya Uhamiaji Uganda - baadhi ya Waganda walikuwa wakidanganya kuhusu pasipoti zao kupotea na kuziuza kwa wahalifu.

Na kuanzia sasa, ofisi za ubalozi yatatumika tu kwa ajili ya kuchukua hati ambazo taarifa zake zimeshapatikana kutoka nyumbani.




Share: