Serikali ya uganda imeamrisha wizara na mashirika ya umma kuanzisha mazoezi ya kila wiki.

Serikali imesema ni kwa ajili ya kupunguza magonjwa yanayohusiana na hali ya maisha.

Maagizo haya yalitolewa baada ya ripoti ya uchunguzi wa demografia na afya ya Uganda ambayo ilionyesha kuongezeka kwa unene kutoka asilimia 17 hadi 26 kati ya mwaka 2006 hadi 2022.

Serikali ya Uganda imeamrisha wizara, na mashirika ya umma kuanzisha mazoezi ya kila wiki.

Serikali imesema ni kwa ajili ya kupunguza magonjwa yanayohusiana na hali ya maisha.

"Hii ni kuwaarifu kutenga masaa mawili kila wiki katika taasisi zenu kwa jili ya kuhimiza afya njema," barua hiyo kutoka kwa Lucy Nakyobe mkuu wa huduma ya umma ilisema, " Mchukulie suala hili kwa umakini."

Uzito kupita kiasi na unene unahusishwa na hatari ya magonjwa ya kawaida kama vile ugonjwa wa kisukari, moyo na saratani.

Utafiti katika taasisi ya saratani ya Uganda umeonya katika ripoti ya mwaka 2022 kwamba changamoto ya saratani nchini Uganda inaweza kuongezeka kwa karibu asilimia 40 ifikapo 2030 kutokana na mabadiliko ya hatari na ukuaji wa idadi ya watu.

Share: