Serikali ya nigeria kuagiza mabenki na mitandao ya simu kuandaa mifumo yake ili ianze kukata tozo za miamala kuanzia mei 20, 2024

Tangazo la Benki Kuu ya Nigeria (CBN) limezitaka Taasisi zote zinazojihusisha na masuala ya Utunzaji Fedha kukata 0.5% ya kila Muamala

Siku chache baada ya Serikali kuagiza Mabenki na Mitandao ya Simu kuandaa Mifumo yake ili ianze kukata Tozo za Miamala kuanzia Mei 20, 2024, Wananchi wamepinga Tozo hiyo na kueleza kuwa itawaongezea ugumu wa maisha

Tangazo la Benki Kuu ya Nigeria (CBN) limezitaka Taasisi zote zinazojihusisha na masuala ya Utunzaji Fedha kukata 0.5% ya kila Muamala kwa lengo la kutafuta pesa za kuimarisha Usalama wa Mtandao

Umoja wa Vyama vya Wafanyakazi na Umoja wa Kutetea Haki za Kijamii, Uchumi na Uwajibikaji (SERAP) wametoa tamko la kupinga utekelezaji wa Tozo hiyo huku wakieleza kuanza hatua za kuishtaki Serikali

Share: