Serikali inatarajia kuongeza huduma ya matumizi ya gesi asilia kwa wakazi wa dar es salaam

Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amesema Serikali inatarajia kuongeza huduma ya matumizi ya Gesi Asilia kwa wakazi wa Dar es Salaam na tayari kuna mpango wa kuifikisha katika nyumba 10,000 Jijini hapo.

Ameongeza "Serikali kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) imesambaza Miundombinu ya Gesi Asilia katika Nyumba 880 za Dar, imejenga Bomba la Gesi lenye urefu wa Kilometa 12.4 kutoka Mwenge hadi Mbezi Beach kupitia Barabara ya Bagamoyo na tayari Viwanda viwili na Hoteli sita vimeunganishwa na Bomba hilo"

Ametoa maelezo hayo Bungeni baada ya Mbunge wa Kawe, Josephat Gwajima, kuhoji lini Serikali itaweka Bomba la Gesi kila Nyumba kwa Wakazi wa Dar ili Wananchi wapate Nishati nafuu.

Share: