Senegal: waandamanaji kumshinikiza rais macky sall kufanya uchaguzi mkuu kabla ya mwezi aprili

Maandamano hayo yameendelea kwa zaidi ya mwezi mmoja ikiwa ni tangu Rais Sall atangaze kuahirisha Uchaguzi Mkuu

Mamia ya Waandamanaji wameripotiwa kuendelea na maandamano ya kumshinikiza Rais Macky Sall kufanya Uchaguzi Mkuu ndani ya mwezi mmoja kabla ya muda wa Urais wake kumalizika Aprili 2, 2024

Maandamano hayo yameendelea kwa zaidi ya mwezi mmoja ikiwa ni tangu Rais Sall atangaze kuahirisha Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika Februari 25, 2024 na badala yake kusogeza mbele hadi Desemba 15, 2024, muda ambao ulibatilishwa na Baraza la Katiba

Baadhi ya madai ya Waandamanaji ni kuachiwa kwa Kiongozi wa Upinzani, Ousmane Sonko. Wiki iliyopita, Rais Sall aliunda kikosi cha Maridhiano ambacho kilipendekeza Uchaguzi ufanyike Juni 2024, hata hivyo Upinzani umegomea pendekezo hilo

Share: