Senegal: rais bassirou diomaye faye amemtaja kiongozi wa chama kikuu cha upinzani kuwa waziri mkuu wake

Rais mpya wa Senegal, Bassirou Diomaye Faye, amemtaja kiongozi wa chama kikuu cha upinzani kuwa waziri mkuu wake.

Ousmane Sonko ni mshauri wa kisiasa wa Rais Faye na wawili hao walikuwa wamefungwa muda mfupi kabla ya uchaguzi wa Machi.

Walipewa msamaha, pamoja na wafungwa wengine wengi wa kisiasa, na Rais anayemaliza muda wake Macky Sall."

Saa chache baada ya kuchukua madaraka kama rais wa Senegal, mheshimiwa Faye amemteua Sonko kuwa waziri mkuu," ofisi ya rais ilichapisha kwenye X.

Awali Bw Sonko alikuwa ametajwa kuwa mgombea urais wa upinzani hadi alipokamatwa na kuamuliwa kuwa hana sifa ya kugombea nafasi hiyo - hatua iliyozua maandamano makubwa.

Wakati wa kampeni wagombea wote walielezea mageuzi makubwa ya kisiasa na kiuchumi, ikiwa ni pamoja na maridhiano ya kitaifa baada ya miezi kadhaa ya misukosuko iliyosababishwa na kufungwa kwao jela.

Katika hotuba yake ya kuapishwa siku ya Jumanne, Rais Faye alisema Senegal itakuwa nchi ya matumaini yenye demokrasia iliyoimarishwa.

Share: