Afrika kama kivutio cha pamoja cha utalii kwa bara ambalo bado linategemea asilimia 60 ya watalii wake kutoka nje ya Afrika
Rwanda imekuwa taifa la karibuni kabisa barani humo kutangaza hatua ya aina hiyo inayolenga kukuza usafiri huru wa watu na biashara kama ilivyo katika kanda ya Schengen barani UIaya.
Rais Paul Kagame ametoa tangazo hilo katika mji mkuu wa Rwanda, Kigali, ambako aliuelezea uwezo wa Afrika kama kivutio cha pamoja cha utalii kwa bara ambalo bado linategemea asilimia 60 ya watalii wake kutoka nje ya Afrika, kwa mujibu wa data kutoka Tume ya Kiuchumi ya Umoja wa Mataifa kwa Afrika.
Hatua hiyo itakapoanza kutekelezwa, Rwanda itakuwa ni nchi ya nne ya Kiafrika kuondoa masharti ya kusafiri kwa Waafrika. Nchi nyingine zilizotoa visa kwa raia wa Kiafrika ni Gambia, Benin na Ushelisheli.
Rais wa Kenya William Ruto alitangaza mapema wiki hii mipango ya kuwaruhusu Waafrika wote kusafiri bila visa kwenda katika taifa hilo la Afrika Mashariki ifikapo Desemba 31 mwaka huu.