Paul Kagame pia anakataa kuthibitisha uwepo wa Wanajeshi wa Rwanda kwenye ardhi ya jirani yake, licha ya kulaumiwa zaidi
Katika mahojiano maalum na FRANCE 24, Rais wa Rwanda Paul Kagame amezungumzia uhusiano uliopo kati ya nchi yake na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo akibainisha kuwa nchi yake iko tayari kuingia vitani na jirani yake ambaye DR Congo.
Katika kujibu shutuma za hivi hivi karibuni kutoka kwa mwenzake wa Congo, Félix Tshisekedi, ambaye kulingana na Rwanda inapanga “mauaji ya halaiki” Mashariki mwa DRC, Paul Kagame anamtuhumu Rais Félix Tshisekedi kwa kupanga kurejea kwa itikadi ya mauaji ya kimbari mashariki mwa DRC, ikilenga Watutsi wa Congo.
Paul Kagame pia anakataa kuthibitisha uwepo wa Wanajeshi wa Rwanda kwenye ardhi ya jirani yake, licha ya kulaumiwa zaidi moja kwa moja na nchi za Magharibi, akithibitisha kwamba lazima ahoji sababu za msingi kuhusu shutuma hizo.
Rais huyo wa Rwanda na mgombea kwa muhula wa nne wa Urais, anakanusha kuwa uchaguzi wa Rais uliopangwa kufanyika Julai 15 ukurasa umeshafungwa ambapo pia anajibu kwa mara ya kwanza shutuma kutoka kwa Muungano wa vyombo vya habari serikali ikishutumiwa katika ukandamizaji na mauaji dhidi ya wapinzani nchini Rwanda na nje ya nchi.