Rupert murdoch amevuta jiko kwa mara ya kwa mara ya tano katika sherehe iliyofanyika california

Mmiliki tajiri wa vyombo vya habari duniani, Rupert Murdoch amevuta jiko kwa mara ya kwa mara ya tano katika sherehe iliyofanyika katika shamba lake la mizabibu huko California.

Murdoch mwenye umri wa miaka 93 amefunga ndoa hiyo jana Jumamosi na mkewe mpya Elena Zhukova mwenye umri wa miaka 67 ambaye ni mwanabiolojia mstaafu wa Urusi.

Kwa mujibu wa ripoti Bw. Murdoch alimchumbia Bi Zhukova punde tu baada ya uchumba wake na mnasihi wa zamani wa polisi Ann Lesley Smith kusitishwa ghafla Aprili 2023.

Bw. Murdoch mzaliwa wa Australia, ambaye ana watoto sita, ni mwenyekiti mstaafu wa News Corporation, ambayo inamiliki Fox News, Wall Street Journal, Sun na Times.


Alijiuzulu kama mwenyekiti wa Fox na News Corp mwaka jana, na kumwacha mtoto wake Lachlan kuongoza kampuni zote mbili.

Murdoch na Bi. Zhukova inasemekana walikutana kwenye tafrija iliyoandaliwa na mmoja wa wake zake wa zamani, mjasiriamali mzaliwa wa China Wendi Deng.

Wenzi wake wengine wa zamani ni mhudumu wa ndege wa Australia Patricia Booker, mwandishi wa habari mzaliwa wa Scotland Anna Mann, na mwanamitindo na mwigizaji wa Marekani Jerry Hall.

Bi Zhukova hapo awali aliolewa na bilionea wa mafuta wa Urusi Alexander Zhukov, huku binti yao Dasha, msosholaiti na mfanyabiashara, aliolewa na tajiri wa Urusi Roman Abramovich hadi 2017.

Share: