Rochelle akamatwa kwa Ufisadi na kuwanyanyasa watoto kingono

Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 64 kutoka Pittsburgh, Rochelle Stewart anakabiliwa na mashtaka kadhaa, yakiwemo unyanyasaji wa kingono na ufisadi wa watoto, baada ya kudaiwa kujaribu kuwanyanyasa kingono wavulana wawili aliowaajiri kufyeka nyasi .

Hata hivyo, wote wawili walimshutumu kwa kuwa na tabia isiyofaa, Mnamo Januari 8, polisi walijibu ripoti ya Stewart kwamba kulikuwa na wizi katika nyumba yake, lakini badala yake wakawakuta wavulana hao ambao walionekana kulewa na kudai kuwa #Stewart aliwapa pombe na kuwafanyia vitendo vya hovyo.

Wavulana hao walisema walipewa dola 5 kufyeka barabara yake ya gari, kisha Stewart akawakaribisha ndani kwa ajili ya chocolate na pombe.

Walidai kuwa Stewart alikaa karibu nao kwenye sofa na kuweka mguu wake juu ya mmoja wa wavulana hao, akimgusa mabegani na miguu kabla ya kuhamia kwenye sehemu zake za siri, kitendo ambacho mvulana mwingine alidaiwa kurekodi kwenye video.

Stewart alikana kwamba wavulana hao walikuwa ndani ya nyumba yake, lakini polisi walipata ushahidi uliothibitisha vinginevyo, ikiwa ni pamoja na koti la mmoja wa wavulana hao na chupa ya vodka yenye nusu ya pombe ndani.

Stewart alikamatwa, akaweka dhamana, na amepangwa kufikishwa Mahakamani Januari 22

Share: