Hakuna hadithi nyingine zaidi ya Wewe kupata haki yako, Muhimu Njoo na Nyaraka zako zote na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda yupo tayari kukuhudumia na kupambana kwaajili yako dhidi ya wanaozuia haki yako kwa muda mrefu.

Mkuu wa Mkoa Mhe. Paul Christian Makonda anakualika na kukusihi usiwe mnyonge kwasababu haki yao inakwenda kupatikana kupitia Mawakili na Wanasheria wabobezi walioandaliwa kukusikiliza na kuhakikisha unaipata haki yako kikamilifu.

Ni fahari na Heshima kwa Mkuu wa Mkoa wetu Mhe. Paul Christian Makonda kukuhudumia na kupambana kuhakikisha unaipata Haki yake na kuyafuta Machozi yako. Ni Kheri pia kukuhudumia wewe Mkazi wa Arusha Popote Pale Ulipo.

Karibu Kwenye Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Arusha kuanzia majira ya saa Mbili asubuhi ili uhudumiwe na kufutwa Machozi kutokana na Haki unayoistahili na kwa bahati mbaya ilifichwa, kukandamizwa na kupokwa na watu wasiokutakia mema.

Kazi ni Moja tu kwa siku tatu mfululizo, kukusikiliza na kurejesha Haki yako iliyopotea.

Share: