Rc makonda amrejeshea massawe ardhi yake iliyouzwa mara mbili

Bwana Godwoshington Mariki na Bwana Dominic Massawe wamekubaliana kumaliza mgogoro wa ardhi ambao walikuwa nao uliotokana na muuzaji kuuza kiwanja chake kwa wanunuzi wawili kwa Nyakati tofauti.

Kulingana na maelezo waliyoyatoa wakati wa Kliniki ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda inaelezwa kuwa Bw. Dominic Massawe ndiye aliyekuwa mnunuzi wa awali kulingana na mkataba wao wa Mei 14, 2019.

Pande zote mbili kwenye Ofisi ya Mkuu wa mkoa Mei 09, 2024 zimekubaliana kwamba muuzaji amrudishie mnunuzi kiwanja chake alichokuwa amemuuzia awali kama walivyokuwa wamekubaliana na kwamba mnunuzi amekubali kurudishiwa kiwanja chake kutoka kwa muuzaji.

Kiwanja hicho kimerejeshwa chini ya usimamizi wa mtoa msaada wa kisheria Wakili George Steve Njohoka ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Mawakili Kanda ya Arusha pamoja na maafisa kutoka Ofisi ya Mkuu wa mkoa na viongozi wa Kata na Mtaa kunapopatikana kiwanja hicho.

Share: