Rc chalamila asaini makubaliano ya awali ya mashirikiano kati ya dsm na jimbo la shaanxi- china

RC Chalamila akiongea na Waandishi wa Habari amesema amepokea ujumbe wa zaidi ya watu 30 kutoka jimbo la Shaanxi-China ambao lengo lao hasa ni kufanya makubaliono ya mashirikiano

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila amesaini makubaliano ya awali ya mashirikiano kati ya Mkoa wa Dar es Salaam na Jimbo la Shaanxi-China katika Ukumbi wa Hotel ya Johari Rotana Ilala Jijini Dar es Salaam. 

RC Chalamila akiongea na Waandishi wa Habari amesema amepokea ujumbe wa zaidi ya watu 30 kutoka jimbo la Shaanxi-China ambao lengo lao hasa ni kufanya makubaliono ya mashirikiano katika nyanja mbalimbali katika Mkoa huu, ambapo kilichofanyika leo ni kusaini (Intention to Cooperation) ambayo kwa kiswahili ni hatua za awali za kuonyesha makubaliano ya kuanza mashirikiano kati ya Mkoa wa Dar es Salaam na Jimbo la Shaanxi nchini China.

Baadaye hatua itakayofuata ni kusaini "MOU-Memorandum of Understanding" ni nyaraka ya kisheria ambayo lazima ipitishwe kwa Mwanasheria wa Serikali kwa ajili ya "Verting" atakaporidhia ndipo tutarudi tena kusaini nyaraka hiyo.

Aidha RC Chalamila amefafanua sababu za kufanya makubaliano hayo ni kwa kuwa Mkoa huo unakua kwa kasi na imekisiwa ifikapo 2030 Dar es Salaam itakuwa moja kati ya "Metropolitan Cities" za Afrika ambapo kwa sasa ziko sita ya saba itakuwa DSM " Mkoa wetu ni lango la kibiashara, Jiji la kidiplomasia, Jijini la kiuchumi ndio maana tumeona umuhimu wa kufanya mashirikiano na Jimbo la Shaanxi-China ambako ndiko makao makuu ya Serikali ya Nchi ya China yaliko" Alisema RC Chalamila

Ifahamike kuwa kutokana na makubaliano hayo yatakwenda kufungua fursa katika Mkoa wetu ikiwemo wimbi kubwa la wafanyabishara na wawekezaji kutoka china, fursa ya kutanua masoko ya bidhaa za kitanzania pia hii inaashiria kutii maelekezo ya Mhe Rais Dkt Samia Suluhu ya kufungua fursa za uwekezaji katika Mkoa kwa masilahi mapana ya Wananchi wa Mkoa huu na Taifa la Tanzania kwa ujumla.

Share: