Rc chalamila aridhia mapendekezo ya ugawaji wa baadhi ya kata na mitaa kigamboni

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila 2023 ameridhia ombi la kugawa maeneo ya Kiutawala katika Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni Kama yalivyowasilishwa Mhe. Chalamila amesema mchakato huo umefuata hatua zote stahiki ikiwa ni pamoja na kutembelea maeneo husika na kutembelea wananchi na viongozi Kisha kufanya mahojiano nao Hata hivyo, RC Chalamila Amepokea maoni mbalimbali ya Wajumbe hao ambapo kwa Umoja wao wamedhihirisha kuwa Kigamboni kwa sasa Ina ongezeko kubwa la watu wanaohamia kutoka sehemu mbalimbali za nchi yetu.

Vile vile Mhe.Mkuu wa Mkoa amesema utekelezaji wa Jambo hili utasaidia kupanua Maeneo ya kiutawala ya Kigamboni ambapo wananchi watapunguziwa umbali wa kwenda kupata huduma mbalimbali, Ikumbukwe kuwa Halmashauri hiyo kutokana na ukubwa wake na uhamiaji wa watu halmashauri hiyo imeona ni vema kuongeza idada ya kata kutoka 9 hadi kata 14 na Mitaa 67 hadi 77 ikiwa ni ongezeko la Kata 5 na Mitaa 10.

Share: