
Volodymyr Zelenskyy amemshukuru Rais Donald Trump kwa ahadi yake ya msaada wa kijeshi, hususan utoaji wa vifaa kama mfumo wa ulinzi wa anga Patriot pamoja na ushauri wa kijasusi. Zelenskyy pia ameonyesha shukrani kwa hatua za wazi kuhusu vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Russia...
Rais Volodymyr Zelenskyy wa Ukraine amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na Rais Donald Trump wa Marekani usiku wa kuamkia leo na kumshukuru kwa utayari wake wa kuendelea kuiunga mkono Ukraine katika vita dhidi ya Urusi.
saa chache baada ya Trump kutangaza mpango wa kuipatia Ukraine silaha zaidi za kujilinda na kuionya Moscow kuwa itakabiliwa na mbinyo wa kiuchumi iwapo vita vitaendelea.
Trump amesema Washington itapeleka silaha za kisasa nchini Ukraine ikiwemo mifumo ya ulinzi chapa Patriot, kupitia washirika wake wa Ulaya.
Pia ametishia kwamba ataziwekea ushuru wa asilimia 100 nchi zinazofanya biashara na Urusi iwapo mkataba wa amani hautapatikana ndani ya muda wa siku 50.