RAISI WA MAREKANI NA WAZIRI MKUU WA ISRAEL KUSITISHA MAPIGANO YA GAZA

Rais wa Marekani Donald Trump amekutana na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kwa mara ya pili ndani ya saa 24 kujadili makubaliano ya kusitisha mapigano Gaza, huku mazungumzo hayo ya ghafla yakifanyika Jumanne jioni katika Ikulu ya White House.

Mazungumzo hayo yaliyodumu kwa zaidi ya saa moja yalifanyika bila kuwepo kwa vyombo vya habari, na yamejiri wakati ambapo wanajeshi wa Israel wamewaua Wapalestina wasiopungua 95 katika Ukanda wa Gaza. Hii ni mara ya tatu kwa Netanyahu kuzuru Marekani tangu Trump aanze muhula wake wa pili tarehe 20 Januari.


Akizungumza kabla ya mkutano huo, Trump alisema kuwa mazungumzo hayo yangehusu Gaza pekee:“Tunalazimika kutatua hilo. Gaza ni janga. Anataka lipate suluhisho, nami pia nataka, na naamini hata upande wa pili wanataka,” alisema Trump.

Wakati huohuo, mjumbe maalum wa Trump katika Mashariki ya Kati, Steve Witkoff, alisema kuwa Israel na Hamas wanakaribia kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano na Washington inatarajia mkataba huo ukamilike kabla ya mwisho wa wiki.


“Tunatumaini kuwa kufikia mwishoni mwa wiki, tutakuwa na makubaliano yatakayosababisha kusitishwa kwa mapigano kwa siku 60. Mateka 10 walio hai wataachiwa, pamoja na miili ya mateka tisa waliokufa,” Witkoff aliwaambia waandishi wa habari wakati wa kikao cha Baraza la Mawaziri.

Hata hivyo, Netanyahu, alipokutana na Spika wa Bunge la Marekani linalodhibitiwa na Republican, alisema kuwa operesheni ya Israel Gaza haijamalizika.


Share: