Rais william ruto ameutuhumu utawala wa rais mstaafu uhuru kenyatta

Rais William Ruto ameutuhumu Utawala wa Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta kuwa ulitenga Bajeti maalum kwaajili ya kuwahonga na kuwarubuni Majaji na Mahakimu ili wawe wanatoa maamuzi ya kuipendelea Serikali.

Amesema Serikali yake haiwezi kuyumbishwa na Kesi zinazofunguliwa katika Mahakama nchini humo kupinga utekelezwaji wa baadhi ya Sera na Sheria na kuongeza kuwa anaheshimu Uhuru wa Mahakama ingawa Uhuru huo huapaswi kuvuruga maslahi ya umma.

Serikali ya Ruto imekuwa ikikumbana na Vikwazo vya Mahakama ikiwemo uzuiaji wa baadhi ya Sheria ikiwemo Sheria ya Fedha ambayo imelalamikiwa na Wananchi kwamba inaongeza Gharama Kubwa za Maisha bila kuzingatia uhalisia wa vipato vyao.

Share: