Rais william ruto amependekeza wabunge wa bunge la (eala) kumuunga mkono raila odinga

Rais William Ruto amependekeza Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) kumuunga mkono Waziri Mkuu wa zamani na Kiongozi wa Upinzani, Raila Odinga anayewania nafasi ya Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AUC)

Akihutubia kikao cha EALA, Rais Ruto amesema Viongozi Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wamekubaliana kuwa Ukanda huu utatoa Mgombea mmoja kwaajili ya Uchaguzi utakaofanyika Januari 2025

Odinga aliyeonesha nia ya kutaka Uenyekiti wa AUC amesema ana imani ya kushinda nafasi hiyo akidai hadi sasa Marais 7 kutoka Afrika wameonesha kumuunga mkono

Share: