Rais william ruto amelishutumu Shirika la ford foundation kwa kufadhili ghasia wakati wa maandamano kenya

Rais William Ruto ameushutumu Ford Foundation, ambalo ni Shirika binafsi la nchini Marekani, kwa kufadhili ghasia wakati wa maandamano dhidi ya serikali.

Akiongea mjini Nakuru siku ya Jumatatu, Ruto alidai kuwa shirika hilo lilikodi watu ili kusababisha ghasia wakati wa maandamano yaliyosababisha uharibifu wa mali na uporaji wa biashara.

"Nataka niulize watu wa Ford Foundation watuambie hio pesa wanatoa, wanatoa ifanye fujo ndio wapate faida gani?"

"Tutawaita na tutawaambia kama hawapendi demokrasia nchini Kenya, kama watafadhili vurugu na machafuko tutawaita na tutawaambia wao pia kujirekebisha au waondoke." Alisema Rais Ruto.

Alisema kuwa serikali yake haitamwacha yeyote anayewasajili vijana wa Kenya ili kusababisha ghasia barabarani wakati wa maandamano ya amani.

Share: