Rais wa zamani wa afrika kusini jacob zuma amezuiwa kushiriki uchaguzi wa mei 2024

Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma amezuiwa kushiriki uchaguzi wa Mei 2024 kutokana na hatia yake ya awali.

Tume ya uchaguzi ya Afrika Kusini ilisema siku ya Alhamisi kwamba imezuia Rais wa zamani Jacob Zuma kugombania nafasi ya rais katika uchaguzi mkuu wa Mei 29.

"Katika kesi ya Rais wa zamani Zuma, ndio, tulipokea pingamizi, ambalo limekubaliwa," Rais wa tume Mosotho Moepya aliwaambia waandishi wa habari, bila kutoa maelezo.

"Chama kilichomteua kimearifiwa" pamoja na wale wanaopinga hatua hiyo, aliongeza.

Uamuzi huo unaweza kukatiwa rufaa ikiwa utawasilishwa kabla ya Aprili 2.





Share: