Rais wa marekani atangaza vita juu ya kundi la islamic resistance linalofadhiliwa na iran

Kundi la wapiganaji wanaosaidiwa na Iran ladai kuhusika na Shambulio dhidi ya Marekani.

Kundi la Islamic Resistance nchini Iraq limesema ndilo lililohusika na shambulio hilo kwenye kambi ya Marekani karibu na mto Jordan na Syria.

Kundi hilo liliibuka mwishoni mwa 2023 na lina wanamgambo kadhaa wenye uhusiano na Iran wanaofanya kazi nchini Iraq.

Pia limedai litatekeleza mashambulizi mengine dhidi ya vikosi vya Marekani katika wiki za hivi karibuni.

Katika taarifa yake kundi la Islamic Resistance limesema lililenga vituo vitatu vya Marekani nchini Syria na Jordan - Shaddadi, Rukban na Tanf, pamoja na kituo cha mafuta cha Israel katika bahari ya Mediterania.

Iran imekanusha kuwa ilihusika na mashambulizi hayo, ikisema "haikuhusika katika maamuzi ya makundi ya upinzani".

Rais wa Marekani Joe Biden alijibu mashambulizi hayo akisema kuwa Marekani "itawawajibisha wale wote waliohusika kwa wakati na namna tutakavyochagua".

Huu ni mfumo wa Iran Wamefadhili na kutoa mafunzo kwa wanamgambo wanaofanya kazi katika eneo hilo, ikiwa ni pamoja na Iraq na Syria.

Maadui wa Iran wanawachukulia kama mtandao wa magaidi, lakini Iran inawachukulia kama ulinzi wake ambao unaweza kuwapiga maadui zao.

Na bado inakataliwa. Wanakanusha kuwa hawakuhusika na shambulio hilo kwenye kambi ya Marekani.

Marekani haikubali hilo. Kwa hivyo shida ya Rais Biden sasa ni jinsi ya kulipiza kisasi, nani apige na wapige wapi.

Kushambulia ardhi ya Iran kutachochea hali, kwa hivyo labda hawataki kufanya hivyo, lakini wanaweza kujaribu kufanya kitu.

Share: