Hafla hiyo ilihitimishwa kwa makubaliano ya pamoja kutoka kwa nchi za Afrika kupanua kwa haraka nishati mbadala katika muongo ujao
Jarida la Time limemtaka rais wa Kenya William Ruto kuwa miongoni mwa watu 100 walio na ushawishi mkubwa zaidi duniani mwaka wa 2024.
Ruto aliibuka kama sauti kuu ya matarajio ya hali ya hewa ya Afrika na kutambuliwa kwa kuandaa mkutano wa kilele wa hali ya hewa mjini Nairobi Septemba mwaka jana, ambao uliwavutia viongozi kutoka kote ulimwenguni.
Hafla hiyo ilihitimishwa kwa makubaliano ya pamoja kutoka kwa nchi za Afrika kupanua kwa haraka nishati mbadala katika muongo ujao, kwa kusaidiwa na dola bilioni 23 (Sh3 trilioni) katika ahadi za kuchochea malengo ya hali ya hewa ya bara.
Jarida la Time lilitaja wito wa Ruto kwa wakopeshaji kupunguza mzigo wa madeni unaokabili baadhi ya nchi za Kiafrika, hivyo basi kufungua milango ya matumizi katika kutatua matatizo ya hali ya hewa kama jambo ambalo limeibua mjadala wenye tija.