Rais wa israel akanusha kuwa hospitali ya gaza imeshambuliwa

Rais wa Israel Isaac Herzog amekanusha kuwa Israel inashambulia hospitali kubwa zaidi ya Gaza.

Ripoti kutoka kwa wafanyikazi wa Al-Shifa zinaonyesha kuwa kituo hicho kinachohifadhi maelfu ya Wapalestina hakina umeme.

Lakini Bw Herzog alisema "kila kitu kinaendelea" hospitalini.

Akizungumza na mwandishi wa BBC Laura Kuenssberg pia alisema nakala ya kitabu cha Adolf Hitler kwa jina Mein Kampf kilipatikana kwenye mwili wa mpiganaji wa Hamas kaskazini mwa Gaza.

Bw Herzog alisema nakala iliyotafsiriwa kwa Kiarabu ilipatikana "siku chache tu zilizopita" katika chumba cha watoto ambacho "kimegeuzwa kuwa kituo cha operesheni ya kijeshi cha Hamas".

Ilani ya kiongozi wa Nazi ya kupinga Uyahudi ilichapishwa kwa mara ya kwanza mnamo 1925.

Akitafuta nakala yake kaskazini mwa Gaza, Bw Herzog alisema, ilionyesha kwamba baadhi ya Hamas "walijifunza tena na tena itikadi ya Adolf Hitler ya kuwachukia Wayahudi".

Awali, Shirika la Afya Duniani (WHO) lilisema limepoteza mawasiliano na hospitali ya Al-Shifa, huku wafanyakazi na wagonjwa wakiwa wamenaswa na mapigano nje.

Share: