Rais wa guinea-bissau amemfuta kazi waziri mkuu geraldo martins

Rais wa Guinea-Bissau Umaro Sissoco Embaló amemfuta kazi Waziri Mkuu Geraldo Martins, wiki moja tu baada ya kumrejesha kwenye wadhifa huo.

Bw Martins aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu kwa mara ya kwanza mwezi Agosti, lakini alipoteza nafasi hiyo mapema mwezi huu wakati Rais Embaló alipovunja serikali kufuatia jaribio la mapinduzi lililoshindwa tarehe 1 Desemba.

Rais kisha akamteua tena Bw Martins kama Waziri Mkuu wiki iliyopita.

Amri ya rais iliyotolewa Jumatano ilitangaza kwamba Rui Duarte de Barros, ambaye hapo awali alihudumu kama Waziri Mkuu wa mpito wa taifa hilo la Afrika Magharibi kati ya 2012 hadi 2014, atachukua nafasi ya Bw Martins.

Mwezi uliopita, kulikuwa na mapigano kati ya vikundi viwili vya jeshi katika mji mkuu Bissau wakati Rais Embaló alipokuwa akihudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa wa hali ya hewa wa COP28 mjini Dubai.

Share: