Rais Samia Suluhu Hassan ni mmoja kati ya Marais wawili pekee wa Wanawake barani Afrika

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, Maarufu Mama Samia, ni mmoja kati ya Marais wawili pekee wa Wanawake barani Afrika.

Samia Suluhu Hassan ameweka historia kwa kuwa mwanamke wa kwanza kuwa Makamu wa Rais na hatimaye Rais wa nchi hiyo.

Safari yake ya kuweka historia ilianza rasmi mnamo 2000 kama Mbunge wa viti Maalum na Chama cha Mapinduzi (CCM) katika Baraza la Wawakilishi Zanzibar.

Tangu alipochaguliwa mbunge wa Makunduchi, visiwani Zanzibar licha ya kuwa mgombea pekee wa kike, nyota yake ya uongozi ilizidi kumbeba hadi kuwa mgombea mwenza wa kwanza wa kike katika historia na hivyo kumfanya kuwa makamu wa kwanza wa rais wa kike Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Kufuatia kifo cha ghafla cha Rais John Magufuli, Machi 17, 2021, katiba ya nchi ilimtaka yeye ndio achukue hatamu ya uongozi wa nchi n ahata kuapishwa tarehe 19 Machi, kuwa rais wa kwanza mwanamke nchini Tanzania.

Fahamu zaidi safari yake ya siasa na rekodi mbalimbali alizoweka ndani na nje ya Tanzania.






Share: