Rais samia suluhu hassan amewapokea marais wa nchi na wawakilishi wa viongozi wa nchi za jumuiya ya afrika mashariki

Mkutano wa 23 kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi na Usalama wa Chakula jijini Arusha.

Rais Samia Suluhu Amewapokea Marais wa Nchi na Wawakilishi wa Viongozi wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, kushiriki Mkutano wa 23 kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi na Usalama wa Chakula jijini Arusha. 

Kazi Inaendelea. Kazi ya kutafuta majawabu dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi kwenye upatikanaji wa chakula yanayogusa moja kwa moja uhai wa nchi zetu, watu wetu, maendeleo yetu, na ustawi wetu wa sasa na siku za usoni. 

Katika mjadala huu mbali na kusikia yapi wenzetu wanafanya na yapi tufanye kwa pamoja, sisi kama nchi tunashirikisha yale tunayofanya kwenye eneo hili ikiwemo; kuongeza bajeti kwenye kilimo na mazingira, mafunzo na mikopo kwa vijana, ruzuku na pembejeo kwa wakulima, ushirikishaji wa sekta binafsi, sera na sheria zetu za utunzaji wa mazingira, vyanzo vyetu vya maji na uongezaji wa uwezo wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA).

Share: