Rais samia: baadhi ya viongozi na madiwani wa halmashauri mbalimbali wanahusika katika migogoro ya ardhi

Rais Samia Suluhu Hassan amesema baadhi ya Viongozi wakiwemo Madiwani wa Halmashauri mbalimbali wamekuwa na utaratibu wa kuanzisha Vijiji kwa lengo la kujinufaisha kwenye masuala ya Uchaguzi, hali inayochangia kuibuka kwa migogoro ya Ardhi

Akizungumza baada ya kuwaapisha Viongozi aliowateua Wiki iliyopita, Rais Samia amesema "Tunakwenda Chaguzi za Serikali za Mitaa, wakubwa wakiona wameharibu upande mmoja na Kura hazipo, wanafanya ushawishi wa kuanzisha Vijiji na kuingilia kwenye hifadhi au mkoa mwingine, migogoro ndio inatengenezwa hivyo."

Kutokana na tatizo hilo kuendelea kulalamikiwa na Wadau mbalimbali, Rais Samia ametoa agizo kwa Mamlaka husika kutofanya mabadiliko yoyote ya kuongeza au kupunguza maeneo na kutaka Vijiji vyote vibaki kama vilivyokuwa katika kipindi kilichopita.

Share: