Rais samia awapandisha vyeo makamishna jeshi la zimamoto na uokoaji kutoka makao makuu dodoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan amewapandisha vyeo Naibu Kamishna Athuman Nassa Rwahila na Naibu Kamishna Happiness Francis Shirima kuwa Makamishna wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.

Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemteua Kamishna Athuman Nassa kuwa Kamishna wa Usalama kwa Umma na Happiness shirima kuwa Kamishna wa Oparesheni za Zimamoto na Uokoaji.


Aidha amewapandisha Kamishna Msaidizi Mwandamizi Zabron Muhumha kuwa Naibu Kamishna, Kamishna Msaidizi Mwandamizi Taki Nguzo kuwa Naibu Kamishna, Kamishna Msaidizi Mwandamizi Puyo Nzalayaimisi kuwa Naibu Kamishna, Kamishna Msaidizi Mwandamizi Julishaeli Mfinanga kuwa Naibu Kamishna,

Vilevile Kamishna Msaidizi Mwandamizi Yusuf Semtana kuwa Naibu Kamishna, Kamishna Msaidizi Mwandamizi Christina Sunga kuwa Naibu Kamishna, Kamishna Msaidizi Mwandamizi Goodluck Zelote kuwa Naibu Kamishna, Kamishna Msaidizi Brighton Monyo kuwa Naibu Kamishna, Mrakibu Mwandamizi Fatma Ngenya kuwa Naibu Kamishna na Mrakibu Shomari Salla kuwa Naibu Kamishna.


Kwa upande wake Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (CGF) John Masunga amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwapandisha vyeo Makamishna hao na ametumia nafasi hiyo kuwakumbusha kwamba kupanda cheo ni kuongezewa majukumu ya kazi na hivyo wawe tayari kuzitumikia nafasi hizo.

Naye Kamishna wa Usalama kwa Umma akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Makamishna hao wapya amesema vyeo hivyo ni deni kwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Taifa kwa ujumla na kuwataka Makamishna wenzake kulipa deni hilo kwa kuchapa kazi kwa bidii, nidhamu na weledi zaidi.

Share: