Rais ramaphosa amemfuta kazi mwanauchumi mashuhuri thabi leoka

Bi Leoka amekuwa mchambuzi na mwanauchumi maarufu nchini Afrika Kusini, akihudumu katika bodi kadhaa na pia kuishauri serikali.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amemfuta kazi mwanauchumi mashuhuri katika jopo la washauri huku maswali yakiibuka kuhusu shahada yake ya uzamivu (PhD).

Thabi Leoka amesema chuo cha London School of Economics (LSE) ambacho kilitunuku shahada hiyo lakini waandishi wa habari kutoka mtandaoni Daily Maverick wamesema hawajaweza kupata rekodi yake ya masomo.

Wiki jana, Bi Leoka alikanusha upotoshaji unaohusu elimu yake.

Siku ya Jumatatu, alijiuzulu kutoka bodi za kampuni mbili zinazojulikana.

Kampuni ya uchimbaji madini ya Anglo American Platinum Limited ilisema Bi leoka amejiuzulu wadhifa wake kama mkurugenzi asiye mtendaji "ili kushughulikia afya yake na maswala ambayo amekuwa akikabiliana nayo kuhusiana na sifa zake za kitaaluma".

Kampuni ya simu za mkononi ya MTN SA ilitoa taarifa sawa na hiyo.

Siku hiyo hiyo, aliambiwa kuhusu "kukatishwa uanachama wake mara moja katika Baraza la Rais la Ushauri wa Kiuchumi", msemaji wa Rais Ramaphosa, Vincent Magwenya.

Uanachama wa chombo hicho "hauhitaji uhakiki rasmi", alisema.

Baraza linashauri kuhusu "sera za kiuchumi zinazochochea ukuaji jumuishi", kulingana na tovuti ya rais.

Katika maoni ya awali kwa gazeti la daily Mavereck ambalo lilikua limeomba ushahidi wa kufuzu kwake, Bi Leoka alisema kwamba amekuwa na shughuli nyingi na hakuwa na wakati wa kupata cheti chake cha digrii.

"Siko [Afrika Kusini] kwa muda wote... Nimekuwa katika Hospitali ya Macho ya Miami Bascom Palmer kwa kuwa nina glakoma na tangu wakati huo nimepoteza uwezo wa kuona katika jicho langu la kulia," alisema kwenye chapisho hilo la mtandaoni.

"Pia huna majina yangu kama inavyoonyeshwa kwenye digrii zangu," aliongeza.

Wiki iliyopita, alisema alikuwa karibu kufanyiwa upasuaji.

Pia alisema kuwa amehitimu kwa kutumia jina tofauti ndiyo maana LSE haikuweza kupata ushahidi wa PhD yake ilipoulizwa na waandishi wa habari.

Bi Leoka amekuwa mchambuzi na mwanauchumi maarufu nchini Afrika Kusini, akihudumu katika bodi kadhaa na pia kuishauri serikali.

Alisema kuwa amehitimu kwa kutumia jina tofauti ndiyo maana LSE haikuweza kupata ushahidi wa shahada yake ya uzamivu alipoulizwa na waandishi wa habari.

Bi Leoka amekuwa mchambuzi na mwanauchumi maarufu nchini Afrika Kusini, akihudumu katika bodi kadhaa na pia kuishauri serikali.

Share: