Rais mwinyi awasili arusha kuhudhuria mkutano wa wanahisa wa crdb
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewasili Mkoani Arusha jioni hii Mei 16, 2024 kupitia uwanja mdogo wa ndege wa Kisongo na kupokelewa na Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda aliyeambatana na viongozi wa Chama na serikali pamoja na maafisa wa vyombo vya ulinzi na usalama Mkoa wa Arusha.



Mhe Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi yupo mkoani Arusha, alipopangiwa kuhudhuria mkutano Mkuu wa mwaka wa wanahisa wa Benki ya CRDB, mkutano unaotarajiwa kufanyika Ijumaa Mei 17, 2024 kwenye Ukumbi wa Kituo cha mikutano cha kimataifa Jijini Arusha AICC.

Share: