elimu lazima iende sambamba na nidhamu, nidhamu ni jambo kubwa sana, bila nidhamu aliyepata elimu atapwaya, atakuwa dhaifu, kwani sifa atakayopata ya elimu astashada, stashada au shahada yake itapwaya
Rais Mstaafu wa serikali ya mapindunzi ya Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein amewataka wahitimu wa elimu ya Vyuo vya juu kuzingatia nidhamu katika kuziendeleza taaluma zao kwa kuwa ndio msingi muhimu katika kuzifikia fursa mbalimbali za maendeleo.
Dkt. Shein ameyasema hayo katika Mahafali ya 22 ya Chuo Kikuu Mzumbe, baada ya zoezi la kuwatunuku vyeti wahitimu 4143, ambapo amesisitiza kuwa elimu lazima iende sambamba na nidhamu, bila nidhamu aliyepata elimu atapwaya.
"..zaidi ya hayo elimu lazima iende sambamba na nidhamu, nidhamu ni jambo kubwa sana, bila nidhamu aliyepata elimu atapwaya, atakuwa dhaifu, kwani sifa atakayopata ya elimu astashada, stashada au shahada yake itapwaya" amesema Dkt. Shein
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Mzumbe Dkt. Saida Yahya Othman na Mlau wa Chuo hicho wakatoa nasaha zao kwa wahitimu hao kuzingatia uadilifu mahala pa kazi.