Rais macky sall kufanya mabadiliko ya tarehe ya uchaguzi mkuu

Taarifa kutoka Senegal zimeeleza kuwa Awamu ya Pili ya Rais Sall ilitawaliwa na Ukandamizaji wa Wapinzani wake

Rais Macky Sall amekubali kufanya mabadiliko ya tarehe ya Uchaguzi Mkuu kutoka Desemba 15, 2024 hadi Machi 24, 2024 kutokana na maandamano yanayomtaka kuheshimu muda wake wa kuondoka madarakani. 

Awali, Rais Sall anayetakiwa kumaliza kipindi cha utawala wake kwa mujibu wa Katiba ifikapo Aprili 2, 2024 alipeleka Muswada Bungeni uliosogeza mbele Uchaguzi na kumpa kibali cha kubaki madarakani hadi Desemba 2024, hali iliyozua vurugu Nchini humo. 

Taarifa kutoka Senegal zimeeleza kuwa Awamu ya Pili ya Rais Sall ilitawaliwa na Ukandamizaji wa Wapinzani wake ambapo takriban Watu 1,000 walifungwa jela kwa kumpinga hadharani Kiongozi huyo. 

Share: