Rais joe biden amesema ataheshimu uamuzi wa kisheria wa mahakama baada ya mwanaye kupatikana na makosa matatu ya uhalifu wa bunduki

Rais Joe Biden amesema ataheshimu uamuzi wa Kisheria wa Mahakama baada ya Mwanaye kupatikana na hatia katika Makosa Matatu ya uhalifu wa Bunduki ambaye anakabiliwa na kifungo cha hadi Miaka 25 jela. 


Jopo la Majaji 12 lilimkuta Hunter Biden (54) na hatia ya kusema uongo kuhusu matumizi yake ya Dawa za Kulevya aina ya Cocaine kwenye fomu wakati akinunua Bunduki Mwaka 2018. 

Ushahidi kutoka kwa Mke wake wa zamani, Kathleen Buhle, na mpenzi wa zamani, Zoe Kestan, picha na Video ulithibitisha Hunter mara kwa mara alikuwa akitumia Dawa Za Kulevya, matumizi yaliyoleta athari kwa Marafiki na Familia yake. 

Share: