Rais félix tshisekedi amelaani ghasia zinazoendelea nchini chad

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Félix Tshisekedi amelaani ghasia nchini Chad baada ya shambulio baya kwenye makao makuu ya Shirika la Usalama la Taifa (ANSE).

Watu kadhaa waliuawa katika shambulio hilo la Jumatano.

Bw. Tshisekedi alielezea wasiwasi wake kwamba matukio ya Chad "yana uwezekano wa kuvuruga mchakato wa siasa ya mpito", huku uchaguzi wa urais ukipangwa kufanyika tarehe 6 Mei.

Tshisekedi alielezea mshikamano wake na mamlaka ya mpito nchini.

Aliunga mkono uamuzi wao wa "uchunguzi wa haraka ili kutoa mwanga kamili juu ya matukio husika, kubaini waliohusika" na kuwapeleka mahakamani.

Haya ni maoni ya kwanza makubwa nje ya Chad tangu shambulio hilo linalodaiwa kufanywa, ambalo serikali imelaumiwa na chama cha upinzani cha Socialist Party Without Borders (PSF).

Chama hicho kinakanusha kikisema maafisa wake walikuwepo kutafuta mwili wa mwanachama aliyekamatwa na kisha kuuawa.

Kinawatuhumu wanajeshi kwa kuwafyatulia risasi wanachama wake.

Haya yanajiri huku kukiwa na wasiwasi kuhusu mahali alipo kiongozi wa chama hicho, Yaya Dillo. Kumekuwa na mvutano katika mji mkuu wa Chad N'djamena, huku kukiwa na milio ya risasi katika maeneo kadhaa yakiwemo makao makuu ya chama cha upinzani.

Share: