Rais emmanuel macron amevunja bunge na kuitisha uchaguzi wa ghafla wa wabunge juni 30 na julai 7

Rais Emmanuel Macron amevunja Bunge na kuitisha Uchaguzi wa ghafla wa Wabunge Juni 30 na Julai 7, baada ya Chama chake cha Renaissance kuburuzwa na Chama cha National Rally (asilimia 31.4%) katika Uchaguzi wa Bunge la Umoja wa Ulaya wa Juni 9, 2024  

Chama cha Marine Le Pen kinachopinga Uhamiaji na kuwa na Sera za utaifa kilikadiriwa kupata karibu 31%-32% ya kura, matokeo ya kihistoria ambayo zaidi ya mara mbili ya asilimia ya kura za Chama cha Renaissance, ambacho kilikadiriwa kufikia karibu 15%

Afisa katika Ofisi ya Rais Macron alisema uamuzi wa kuvunja Bunge ulikuwa na sababu ya “matokeo ya kihistoria ya mrengo wa kulia” ambayo yasingeweza kupuuzwa na vurugu za Bunge za sasa

Share: