Rais dkt.mwinyi avuka malengo ya ilani ya ccm

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amejivunia miaka mitatu ya Serikali ya awamu ya nane madarasa 2,273 sawa na asilimia 150 ya malengo ya ilani ya CCM kwa ujenzi wa Skuli mpya Unguja na Pemba hivyo kuvuka malengo ya Ilani ya CCM 2020-2025 iliyoelekeza kujengwa madarasa 1,500 ya Msingi na Sekondari Unguja na Pemba kwa miaka mitano.

Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo alipoweka Jiwe la Msingi la ujenzi wa Skuli ya Sekondari ya Utaani Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba tarehe: 04 Januari 2024 katika shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

Aidha, Rais Dkt.Mwinyi amesema ni matumaini yake uwekezaji unaoendelea kufanywa na Serikali kuimarisha miundombinu katika sekta ya elimu utachochea zaidi ufaulu wa wanafunzi. 

Kwa upande mwingine Rais amemtaka mkandarasi wa ujenzi wa Skuli hiyo Benchmark na Wakala wa Majengo Zanzibar (ZBA) kumaliza ujenzi wa Skuli ya Utaani mwezi Machi mwaka huu na atafika kufungua baada ya kukamilika.

Naye, Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar Dkt. Mohamed Said Dimwa amempongeza Rais Dk.Mwinyi kwa kuvuka malengo ya utekelezaji wa Ilani ya CCM 2020-2025 katika sekta ya elimu nchini.

Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi amelitaka Shirika la Biashara Zanzibar (ZSTC) kuagiza chakula nje kukabiliana na kupanda kwa bidhaa nchini, Serikali italiwezesha shirika hilo kifedha kuagiza chakula nje kuleta ushindani na Wafanyabiashara binafsi kuhakikisha wananchi wanapata chakula kwa bei nafuu kabla ya kuingia Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

Share: