Rais dkt. samia suluhu hassan amewekeza katika mradi wa umwagiliaji wa billion 57 pawaga iringa

VIJANA wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa wametakiwa kujikita katika siasa na uchumi kwa sababu bila kuwa na uchumi imara huwezi kufanya siasa unayoitaka.

Akizungumza wakati Mafunzo kwa Baraza la vijana Wilaya ya Iringa Mjini,Katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa wa Iringa Joseph Ryata amesema Serikali ya Awamu ya sita imekuwa ikitoa fursa nyingi za kiuchumi kwa vijana hivyo ni jukumu la vijana kuchangia fursa hizo.

Ryata amesema kuwa Rais Dkt. Samia suluhu Hassan anatoa mikopo ya asilimia 10 kwenye halmashauri zote nchi nzima ikiwepo Iringa hivyo ni moja ya fursa huku akiitaja fursa ya utalii ambayo kwa sasa mkoa wa Iringa imeshika kasi.

Amesema katika mkoa wa Iringa vijana wana fursa ya kufanya kilimo cha umwagiliaji kwa kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amewekeza Mradi wa umwagiliaji wa billion 57 Pawaga huku wakiendelea kuwatafutia masoko ya nje kwa wakulima wa mazao mbalimbali wa mkoa wa Iringa.

Share: