Rais Dkt.Mwinyi ametoa wito kwa washiriki wa mkutano huo kutembelea vivutio mbalimbali Zanzibar na kujionea maendeleo yaliyofikiwa.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema wajane wanahitaji kutambuliwa rasmi kisheria, kuheshimiwa, kuwezeshwa kiuchumi na huduma bora za Afya.
Rais Dk.Mwinyi ameyasema hayo alipofungua mkutano wa kwanza wa Wajane Afrika katika hoteli ya Golden Tulip uwanja wa ndege Zanzibar tarehe 20 Juni 2024.
Aidha Rais Dkt.Mwinyi ameleeza kuwa mkutano huo utumike kwa kubadilishana mawazo na uzoefu kwa lengo la kujenga muelekeo wa baadae wa nafasi ya wajane katika bara la Afrika.
Rais Dkt.Mwinyi ametoa wito kwa washiriki wa mkutano huo kutembelea vivutio mbalimbali Zanzibar na kujionea maendeleo yaliyofikiwa.