Rais dk. mwinyi amewasili zanzbar hii leo

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.Hussein Ali Mwinyi amerejea Zanzibar baada ya kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan katika Jukwaa la Doha (Doha Forum) ambalo alishiriki ufunguzi wake pamoja na mdahalo wa majadiliano kuhusu kujenga uchumi wa kidijitali.

Baada ya kumalizika Jukwaa hilo alielekea Nairobi, Kenya katika Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru wa Kenya (Jamhuri Day) zilizofanyika uwanja wa Uhuru Gardens ambapo pia alimwakilisha Rais Dkt.Samia katika Sherehe hizo.

Rais Dk. Mwinyi amepokewa na Makamu wa Pili wa Rais Mhe.Hemed Suleiman Abdulllah pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali, Wazee wa Chama na Vyombo vya ulinzi na usalama. 

Katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani leo tarehe:13 Desemba 2023.

Share: