Rais cyril ramaphosa ametangaza tarehe ya uchaguzi mkuu wa kitaifa

Miongoni mwa mambo yanayodaiwa kuwa yatakipa changamoto Chama Tawala ni pamoja na Mgawo mkali wa Umeme

Rais Cyril Ramaphosa ametangaza tarehe ya Uchaguzi Mkuu wa Kitaifa na Majimbo na kueleza kuwa utafanyika Mei 29, 2024 ambapo ameitisha Kikao na Wakuu wa Mikoa pamoja na Viongozi wa Tume kwaajili ya kujadili utekelezaji wa Uchaguzi

Wachambuzi wa Siasa wameonya kuwa Chama Tawala cha African National Congress (ANC) kitakabiliwa na changamoto kubwa ya kutetea Idadi kubwa ya Wabunge katika Uchaguzi wa 7 wa Kidemokrasia Nchini humo tangu kumalizika kwa Mfumo wa Ubaguzi wa Rangi Mwaka 1994

Miongoni mwa mambo yanayodaiwa kuwa yatakipa changamoto Chama Tawala ni pamoja na Mgawo mkali wa Umeme ambao umekuwa ukijirudia, Ukosefu wa Ajira pamoja na mvutano uliopo ndani ya Chama ukichangiwa na Rais aliyejiuzulu, Jacob Zuma

Share: