Raia wa ecuador wamepiga kura ya maoni kama njia ya kukabiliana na magenge ya uhalifu

Raia wa Ecuador wamepiga kura ya maoni kwenye Hatua kadhaa za Kiusalama zinazopendekezwa na Rais wao kama njia ya kukabiliana na Magenge ya Uhalifu yaliyosababisha wimbi kubwa la machafuko.


Maswali mengi waliyoulizwa wapiga kura yanalenga kuimarisha hatua za Usalama ikiwemo kulitumia Jeshi kupambana na Magenge hayo, na kuongeza muda wa vifungo kwa wanaopatikana na hatia ya ulanguzi wa Dawa za Kulevya.

Ecuador imetikiswa katika Mwaka wa hivi karibuni na wimbi la machafuko, ambapo Mwaka jana, kiwango cha mauaji kilifikia hadi vifo 40 kwa kila Watu 100,000.

Share: